Klabu ya Manchester United ipo kwenye hatua za mwisho za kuwaongezea mikataba ya muda mirefu wachezaji wawili ambao ni Marcus Rashford na beki Diogo Dalot.

Wachezaji hao ambao wako mwishoni kumaliza mikataba yao klabu hiyo imeshafanya mazungumzo na nyota hao na kilichobakia ni kuwasainisha ili kuweza kusalia kwenye viunga na Old Trafford na kuitumikia klabu hiyo.RashfordNyota Marcus Rashford atamaliza mkataba wake mwezi Juni mwaka huu kama ilivyo kwa mwenzake Diogo Dalot, Hivo Mashetani wekundu wamewaongezea mkataba wachezaji hao kutokana na ubora ambao wamekua wakiuonesha.

Mshambuliaji Marcus Rashford amekua kwenye kiwango kikubwa siku za hivi karibuni na kuanza kuhusishwa na vigogo wa soka kutoka nchini Ufaransa klabu ya PSG, Hii ni sababu mojawapo ya klabu hiyo kufanya mazungumzo ya kuhitaji nyota huyo kusaini mkataba ndani ya klabu hiyo.RashfordBeki Diogo Dalot ambaye amekua na ubora mkubwa tangu kocha mpya wa timu hiyo Eric Ten Hag afike klabuni hapo, Kutokana na ubora huo na kuonekana ni chaguo la mwalimu klabu imefikia makubaliano ya kumuongezea mkataba mrefu ili aweze kusalia klabuni hapo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa