Manchester United wameanza rasmi mipango ya kuijenga upya timu yao kuelekea msimu mpya baada ya kurejea Champions League, lakini jina la Marcus Rashford linaendelea kutikisa vichwa vya habari Old Trafford huku mustakabali wake ukiwa bado ni mjadala mkubwa.

Nyota huyo wa England ambaye yupo kwa mkopo Barcelona anaonekana kufurahia maisha ya Hispania kiasi cha kuwa tayari kupunguza mshahara wake kwa asilimia 40 ili kuhakikisha anabaki Camp Nou. Ripoti kutoka Hispania zinaeleza kuwa Rashford tayari amekubaliana kwa maneno mkataba wa miaka mitatu na mabingwa hao wa La Liga.
Hata hivyo, dili hilo bado halijafungwa rasmi kutokana na changamoto za kifedha. Barcelona wanataka kubadili mpango wa mkataba huo na kuufanya uwe wa miaka mitano ili waweze kugawanya gharama ya usajili kwa muda mrefu zaidi. Hilo linaonekana kuwa njia yao ya kujaribu kupunguza presha ya fedha ndani ya klabu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa upande wa Manchester United, hawapo tayari kushusha bei ya pauni milioni 26 ambayo ilikuwa imewekwa kama kipengele cha kumnunua moja kwa moja. Barcelona nao wanaonekana kusita kulipa kiasi hicho kwa wakati huu, jambo linalofanya mazungumzo yaendelee kuwa magumu licha ya Rashford mwenyewe kuonyesha wazi anataka kubaki Hispania.

Tangu ajiunge na Barcelona, Rashford ameonekana kufufuka upya akiwa amechangia mabao nane na assist tisa katika mechi 31, huku kiwango chake kikimsaidia Hansi Flick kutwaa ubingwa wa La Liga.


