Rashford pamoja na mchezaji mwezake wa Manchester United Jadon sancho wanatarajia kuitwa tena katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.

Wachezaji hao ambao wameanza msimu vizuri katika klabu yao ya Man United inaelezwa wamemshawishi mwalimu wa timu ya taifa Gareth Southgate kutokana na kiwango walichokionesha hivi karibuni.

rashfordSancho pamoja Rashford hawakua na msimu mzuri kwenye msimu uliomalizika baada ya timu yao kufanya vibaya sana kunako ligi kuu ya Uingereza na michuano mingine na wachezaji hao wakiwa sehemu ya kikosi hicho na hawakuonesha kiwango kizuri hivo kupelekea kocha wa timu ya taifa kuwatema nyota hao kikosini.

Hii ilitokea baada ya michuano ya ulaya kwa timu za taifa wakati timu hiyo ya taifa ya Uingereza ikicheza fainali dhidi ya Italia na kupoteza kwa mikwaju ya penati na nyota waliokosa mikwaju iliopelekea Uingereza kupoteza mchezo huo wachezaji hao walihusika.

Kuanzia hapo na msimu wa 2021/22 ulipoanza haukua mzuri kwa nyota hao na kukosa nafasi kwenye timu hiyo lakini wanaonekana kurudisha makali yao mpaka mechi zilizochezwa sasa kwani Rashford amehusika kwenye magoli matano mpaka sasa akifunga magoli matatu na kusaidia upatikanaji wa mengine mawili kwa upande wa Sancho yeye amefunga magoli mawili mpaka sasa na kuaminika kwenye kikosi cha mwalimu Ten hag kutokana na kuonesha kiwango kizuri.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa