Rasmi Chido Obi Martin ni Mchezaji wa Man United

Kinda wa zamani wa klabu ya Arsenal Chido Obi Martin sasa ni mchezaji rasmi wa klabu ya Manchester United baada ya usajili wake kukamilika kupitia bodi ya ligi kuu ya Uingereza hivo mchezaji huyo anaweza kuanza kutumika kwenye michezo ya timu hiyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka (16) alisajiliwa kwenye dirisha kubwa lililopita ambapo hakua ana uwezo wa kuitumikia timu hiyo bado, Kwani alikua hajakamilisha taratibu za usajili kwenye bodi ya ligi hiyo hivo baada ya kuthibitishwa mapema leo mchezaji huyo anaweza kuanza kuwatumikia Man United.chido obi martinManchester United imemchukua kinda Chido Obi Martin kwa malengo muda mrefu klabuni hapo kutokana na umri wake mdogo tu wa miaka (16) tu, Hivo mchezaji huyo ataendelea kupata nafasi taratibu ndani ya kikosi cha Man United mpaka pale atakapokomaa na kuaminika zaidi kwenye kikosi cha kwanza.

Mshambuliaji Chido Obi Martin ana matumaini ya kupata muda wa kucheza ndani ya Man United kwani aliondoka ndani ya klabu ya Arsenal kwasababu klabu hiyo haitoi kipaumbele kwa vijana wanaotoka akademi miaka ya hivi karibuni, Lakini hali ni tofauti kwa upande wa Man United wao wanatoa nafasi kwa vijana wadogo wanaotoka akademi ya klabu yao.

Acha ujumbe