Klabu ya Manchester United leo imethibitisha kumteua meneja wa Ajax, Erik ten Hag kuwa meneja mpya wao mpya kwa mkataba wa miaka minne.
Baada ya kusaini mkataba huo Ten Hag amesema: “Ni heshima kubwa kuteuliwa kuwa kocha wa Manchester United, ninafuraha kubwa”.
“Ninajua historia ya klabu hii kubwa na shauku ya mashabiki, na nimedhamiria kabisa kuendeleza timu yenye uwezo wa kuleta mafanikio yanayostahili”, Ten Hag aliongeza.
Mkurugenzi wa Manchester United John Murtogh anasema: “Tumefurahishwa sana na maono ya muda mrefu ya Hag ya kuirejesha Manchester United kwenye kiwango tunachotaka kushindana, na ari yake na dhamira yake kufikia hilo”.
Makubaliano ya kazi yanaendelea pia kwa Mitchell van der Gaag kuwa sehemu ya wakufunzi wa Meneja huyo mpya pale Old Trafford, wakitokea Ajax.
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.