Rasmi Klabu ya Watford imeshuka daraja kutoka Ligi ya Primia ikiwa imesalia michezo 3 baada ya kukubali kichapo cha 1-0 kutoka kwa Crystal Palace katika dimba la Selhurst Park Stadium.

Kikosi cha Roy Hodgson kilihitaji kushinda dhidi ya timu yake ya zamani ya Crystal Palace na kutegemea Everton kufungwa [Leo] katika dimba King Power ili kuendelea kuweka matumaini ya kujikwamua kutoshuka daraja.

 

watford, Rasmi Watford Yashuka Daraja EPL., Meridianbet

Wilfried Zaha alididimiza ndoto za Watford kuendelea kujipapatua katika shimo la kushuka daraja baada ya kufunga penati katika dakika ya 31 kipindi cha kwanza kabla ya kamara kutolewa dakika ya 68 kwa adhabu ya kadi nyekundu.

Meneja wa Watford, Roy Hodgson amesema: “Hakukuwa na tofauti kutoka mchezo tuliopoteza wiki iliyopita, tulipofungwa magoli 2 tulikuwa nyuma kwa alama 12 tukiwana na michezo 4 pekee iliyobaki.

“Kwa mtu asiyejua kuhusu mpira ndio anaweza kusema tungeweza kuepuka hili, mechi zote 4 zilizosalia zilikuwa ngumu na timu nyingine zimesalia na michezo mingi ya kucheza.” aliongeza.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa