Rasmus Hojlund Aonekana Mazoezini

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Denmark Rasmus Hojlund ameonekana katika mazoezi ya klabu hiyo katika cha mazoezi ya klabu hiyo Carrington asubuhi ya leo.

Rasmus Hojlund alionekana kupata majeraha katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Luton Town kabla ya mapumziko ya michezo ya kimataifa, Lakini leo ameonekana kurejea Carrington.Rasmus HojlundMshambuliaji huyo alikosa michezo miwili ya timu yake ya taifa ya Denmark katika michezo ya kufuzu mataifa ya ulaya mwak 2024, Lakini alikosa mchezo wa klabu yake ya Man United wikiendi hii dhidi ya Everton.

Raia huyo wa Denmark inaonekana hakupata majeraha makubwa katika mchezo dhidi ya Luton Town katika ligi kuu ya Uingereza, Kwani mchezaji huyo amekaa nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili tu.Rasmus HojlundMshambuliaji Rasmus Hojlund ni wazi atasafiri na kikosi cha Manchester United kuelekea nchini Uturuki katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya ambapo klabu hiyo itakwenda kumenyana na klabu ya Galatasaray mabingwa wa soka nchini humo.

Acha ujumbe