Ratcliffe Kuchelewa Kununua Hisa zake

Taarifa zinaeleza ununuzi wa hisa asilimia 25 ndani ya klabu ya Manchester United kwa tajiri raia wa kimataifa wa Uingereza Sir Jim Ratcliffe huenda ukachelewa mpaka mwanzoni mwaka mpya 2024.

Vyanzo vya ndani ya klabu ya Manchester United vinaeleza kua dili hilo litasogezwa mbele mpaka mwanzoni mwaka ujao 2024, Lakini baada haijajulikana ni sababu gani zimepelekea mchakato huo kusogezwa mbele.ratcliffeWamiliki wa klabu ya Manchester United familia ya Glazer walishakubalina na tajiri Ratcliffe kumuuzia hisa aslimia 25 klabuni hapo na ikafahamika mchakato utamalizika ndani ya mwezi huu, Lakini mambo hayajaenda kama yalivyopangwa na mchakato huo umesogezwa mbele.

Mabadiliko ya uongozi klabuni hapo wiki iliyopita yalitoa taswira ya moja kwa moja kua tajiri huyo atauziwa hisa hizo wakati wowote, Lakini taarifa za mchakato kuchelewa umezua hofu kwa mashabiki wa klabu ya Man United.ratcliffeFamilia ya Glazer wamekua na changamoto katika kuuza klabu hiyo kwani kabla ya Jim Ratcliffe, Sheikh Jassim kutoka Qatar alihitaji kuinunua klabu hiyo kwa asilimia 100 lakini wamiliki hao walikataa ofa yake jambo ambalo linaendelea kuibua hofu zaidi kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao wanaamini wamiliki hao ni sababu kubwa ya klabu hiyo kufanya vibaya.

Acha ujumbe