Ratcliffe: Tunataka kua kama Real Madrid

Bosi mpya wa klabu ya Manchester United Sir Jim Ratcliffe amezungumza leo kua anatamani klabu hiyo ifike kwenye ubora ambao wanao mabingwa wa ulaya na Hispania klabu ya Real Madrid.

Ratcliffe akifanya mahojiano na kituo kimoja cha habari nchini Uingereza ametanabaisha lengo kubwa ndani ya klabu hiyo ni kuhakikisha wanaimarisha maeneo mbalimbali kwenye klabu hiyo kuanzia kwenye uongozi, usajili, lakini pia kuboresha miundombinu ya klabu hiyo ambao wameanza na kuboresha kiwanja cha mazoezi.ratcliffe“Sasa tutahitaji dirisha la usajili la majira ya kiangazi mara mbili au tatu ili kurekebisha mambo,”

“Kila mtu duniani anajua kuhusu Manchester kwa sababu ya Man United. Tunaweza kusema Manchester United ni kama Coca-Cola, sivyo? Kila mtu anajua… hiyo ni kweli.”

“Kuna nafasi ya maboresho kila mahali tunapoangalia hapa Man United na kwa hivyo tutaboresha kila kitu.”

“Tungependa kuwa pale ambapo Real Madrid ipo leo, lakini itachukua muda. Itachukua dirisha la usajili la majira ya kiangazi mara mbili au tatu ili kufika mahali pazuri zaidi.”ratcliffeTangu klabu hiyo ichukuliwe na Sir Jim Ratcliffe imefanya mabadiliko kadhaa kuanzia kwenye uongozi ambapo walimuondoa mkurugenzi mkuu mtendaji klabuni hapo, Mkurugenzi wa michezo, na kufanikiwa kumleta mkuu wa kitengo cha ufundi huku wakipanga kufanya usajili wa maana kwenye dirisha kubwa la mwaka huu.

Acha ujumbe