Bosi wa klabu ya Real Madrid kwa sasa, Mfaransa, Zinedine Zidane anampigia upatu nyota mwenzake aliyeacha heshima kubwa na historia ya aina yake ndani ya kikosi cha Madrid mwamba anaamini siku moja kumuona akiwa ndani ya klabu hiyo aliifundisha soka kama mkufunzi wa soka.
Hayo yamekuja baada ya Zidane kuona kwamba nyota huyo wa zamani ana kila linalohitajika ndani ya kikosi chao kutokana na mapenzi yake ya dhati ndani ya kikosi hicho. Zaidi anaamini uwezo wake haukuwa uwanjani pekee bali ulikuwa hata katika mapambano mengine zaidi ya kuweza kuifanya Madrid ikae sehemu sahihi.
Zidane ambaye kwa sasa ndiye kocha ndani ya kikosi hicho, bado hajapata muunganiko mzuri utakaosaidia kikosi chake hicho kupata ushindi wa wazi katika mechi zenye ushindani mkubwa lakini kutokana na hilo; amekuwa kwenye shinikizo kubwa la hasa endapo ataendelea kupewa muda zaidi kikosini hapo.
Katika mechi kumi ambazo ameweza kutoka nje ya uwanja wake ameweza kupata ushindi wa mechi nne pekee ikiwa ni mafanikio ya chini sana kwa kocha huyo na kikosi hicho alichokisajili. Ikumbukwe alikipokea kikosi hicho na kupata mafanikio makubwa sana lakini hajaweza kuyarudia tangu arejeshwe upya kukinoa tena.
Kipigo chao ndani ya ligi dhidi ya Mallorca kiliongeza shinikizo la hasa endapo nyota huyo wa zamani wa kikosi hicho ataendelea kuaminiwa apewe nafasi zaidi. Lakini makosa hayo tena yakaja kufichwa na ushindi walioupata katika mchezo wa kuwania nafasi za ushiriki ndani ya michuano ya klabu bingwa.
Zidane aliyazungumza hayo katika hafla ya kumpongeza nyota huyo [Raul] kwa kuweza kufikisha miaka 25 tangu aanze kujihusisha na soka. Kwa sasa nyota huyo anafundisha timu ya watoto ya Madrid-Castilla. Na nyota huyo akampa neno la kwamba anaamini nyota huyo atafikia hatua yake ya kupandishwa na kupewa timu kubwa.
Wawili hao wamecheza pamoja huku Raul akiweka rekodi ya kufunga magoli 323 katika mechi 741 alizocheza na klabu hiyo. Ameweza kushinda makombe sita ya ligi na matatu ya klabu bingwa jambo ambalo sio la kubezwa kabisa kwake kwani ni mafanikio makubwa sana kufikiwa.
Gabriel
Habar njema sana 👍