Real Madrid: Alaba Hausiani na Ramos

Waswahili wanakwambia “simba mwendapole, ndiye mlanyama”. Hapa ni Real Madrid katika harakati za kuisaka saini ya David Alaba kutoka Bayern Munich.

Hali ya sintofahamu kuhusu mkataba mpya wa Alaba kubaki Bayern inaendelea kuwapa mwanya Real Madrid kuendelea kufuatia kwa ukaribu mchakato huu.

Alaba atakuwa huru kufanya mazungumzo na klabu yeyote kuanzia Januari 1, 2021 endapo hatakuwa amesaini mkataba mpya (mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu).

Real Madrid na Bayern Munich wanauhusiano mzuri linapokuja suala zima la kufanya biashara ya kubadilishana wachezaji. Xabi Alonso, James Rodriguez, Toni Kroos na Alvaro Odriozola ni miongoni mwa wachezaji waliotoka timu moja kwenda nyingine.

Usajili wa Alaba hauhusiani kwa chochote na hatma ya Sergio Ramos ndani ya kikosi cha Madrid. Ripoti kutoka kwenye ukurasa wa Marca zimesema, Alaba anaonekana kama mtu sahihi wa kuimarisha safu ya ulinzi hasa nafasi ya beki wa kati na hii haihusiani kwa chochote na Ramos.

Endapo Madrid wataipata saini ya Alaba na wakafanikiwa kumbakiza Sergio Ramos, watakuwa wameua ndege wawili kwa jiwe moja. Safu ya Madrid inaonekana kusuasua kwa siku za karibuni na uwepo wa mabeki hawa kwenye safu moja ya ulinzi, itakuwa ni ahueni kwa Zinedine Zidane.

Madrid watafanikiwa katika hili?


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

21 Komentara

    madrid waweke mkwanja mezani tu mbona watampata

    Jibu

    Hapo kikubwa pesa tyu!

    Jibu

    asante meridianbet kwa habar moto moto

    Jibu

    Madridi aweke pesa juu ya meza kiereweke hapo

    Jibu

    Madrid acheni ubahili chukueni jembe hilo.

    Jibu

    Asantee kwa makala

    Jibu

    Hapo kikubwa mkwanja tu

    Jibu

    Alaba yupo vizuri.wangempata ingekua big deal

    Jibu

    Watakuwa wamepata wachezaji sahihi mana hao ni balaa wasiwe wagumu kuweka pesa mezani wapate saini zao tu

    Jibu

    Mkwanja ndio mpango mzima

    Jibu

    Asant kwa taarifa

    Jibu

    Mashabiki tunashuru kwa taarifa

    Jibu

    Money talks

    Jibu

    Kila la kheri kama deal hlo litakamilika alaba kutuwah santiago

    Jibu

    Itakua poa sana akitua madrid

    Jibu

    Watafanikiwa kama watafkiana vizuri maamuzi yao

    Jibu

    Pesa mbele kama tai

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Hapo pesa ndo mpango mzima

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Alaba ,Haaland wako juu sana

    Jibu

Acha ujumbe