Real Madrid Wabadili Gia kwa Eden Hazard

Klabu ya Real Madrid imebadili mawazo kuhusu mchezaji wao nyota Eden Hazard kuhusu hatma yake kwenye klabu hiyo baada ya awali kupanga kumuweka sokoni kwa kutaka kumuuza moja kwa moja.

Eden Hazard hana msimu mzuri kwenye klabu hiyo tokea aliposajiriwa kwa kitita kikubwa akitokea klabu ya chelsea mwaka 2019, huku akiwa anapambana kuweza kurejesha kiwango chake na majeruhi ya mara kwa mara.

Real Madrid

Hata alipokuwa sawa kiafya lakini kocha Carlo Ancelotti amekuwa akiwapa nafasi zaidi Marco Asensio na Rodrygo, hata anapopata nafasi kwenye kikosi cha Real Madrid bado amekuwa akipata tabu kuweza kuwa sawa.

Kwa sasa Eden Hazard yuko nje ya kikosi cha Real Madrid anafanyiwa upasuaji wapili ili kuweza kuondoa kifaa alichowekewa alipovunjika mfupa mwaka jana, na atakosekana kwenye kikosi cha Los Blancos kwa wiki sita.

Klabu ya Real Madrid kwa sasa wamefuta mpango wao wa kutaka kumuuza, bali wanahitaji kumpeleka kwa mkopo wa muda mrefu ili aweze kupata nafasi zaidi ya kucheza. Klabu ambayo itahitaji kumchukua kwa mkopo itabidi wakubali kuchangia mshahara wake.

Real Madrid chanzo cha kufuta kumuuza ni thamani yake sokoni kwa sasa imeshuka, huku kikwazo kikubwa cha kubaki nae ni gharama za mshahara ambazo anavuna ni kubwa mno, na wanahitaji kupunguza gharama za kuweza kumtunza.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe