Klabu ya Real Madrid leo wanacheza mchezo wao wa sita kwenye ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Atalanta mchezo utakaopigwa nchini Italia ambapo mabingwa hao watetezi wa ulaya watakua ugenini dhidi ya vijana wa Gianni Pierro Gasperinni.
Real Madrid wako kwenye wakati mgumu kwenye michuano ya ulaya msimu huu ambapo michuano imekua na mfumo mpya na klabu hiyo mpaka sasa kwenye michezo yao mitano waliyocheza wamepoteza michezo mitatu, Huku wakishinda michezo miwili tu na mpaka sasa wakiwa wanakamata nafasi ya 24 kwenye msimamo wa michuano ya ligi ya mabingwa ulaya.
Msimu huu amekua kwenye ligi ya mabingwa ulaya vijana wa Carlo Ancelotti hawajaanza vizuri kwenye michuano hiyo kwani wameshinda michezo miwili tu kati ya mitano, Huku wakikamata nafasi ya 24 ambayo ndio nafasi ya mwisho ambayo inatoa fursa ya kucheza mtoano ili kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo hivo wakipoteza leo ni dhahiri watashuka na kujiweka kwenye hatari ya kushindwa kucheza hata mtoano.
Hatari kwa Real Madrid leo wanakwenda kucheza na moja ya wapinzani wenye ubora mkubwa kwasasa klabu ya Atalanta kwani klabu hiyo ndio vinara wa ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie, Hivo mchezo huo unatarajiwa kua wenye ushindani mkubwa na mgumu licha ya kua mabingwa hao watetezi wa ulaya waliwafunga Atalanta kwenye mchezo wa Uefa Super Cup mwezi Agosti mwaka huu.
Taarifa nzuri kwa Real Madrid ni kua wanakwenda kwenye mchezo huu wakiwa na nyota wake Vinicius Junior ambaye alikua na majeraha wiki mbili zilizopita, Hivo kurejea kwake itakua ni chachu kwa klabu hiyo kuhakikisha wanapata matokeo mazuri leo angalau kuongeza alama na kusogea nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi hiyo.