Klabu za Real Madrid na Barcelona zimetawala katika tuzo za mchezaji bora kijana chini ya miaka 21 ambayo inafahamika kama Kopa Trophy inayotolewa na jarida la Ufaransa la France Football.

Vilabu vya Real Madrid na Barcelona vimefanikiwa kuingiza wachezaji watano kwenye tuzo hiyo kwa ujumla wake Barcelona wakiingiza watatu ambao ni Pedri, Gavi, na Alejandro Balde Madrid wao ni Jude Bellingham na Eduardo Camavinga.real madridTuzo hizi ambazo zinachukuliwa kama Ballon Dor kwa upande wa vijana ambapo kwa miaka miwili nyuma tuzo hii imekwenda kwa klabu ya Barcelona ambapo wachezaji Pedri na Gavi walifanikiwa kutwaa tuzo hiyo.

Mwaka huu tena wachezaji Gavi na Pedri wamefanikiwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo hiyo, Lakini wakati huu wakiwa hawapewi nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo wakati huu Jude Bellingham na Jamal Musiala wakipewa nafasi kubwa zaidi.real madridMbali na Real Madrid na Barcelona lakini timu zingine zimeweza kuingiza wachezaji wao kama Rasmus Hojlund kutoka Man United, Jamal Musiala kutoka Bayern,Antonio Silva Benfica, Xavi Simons Rb Leipzig, Eyle Wahi Rc Lens.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa