Real Madrid: Usajili wa Mbappé Mashakani.

Baada ya mambo kumuendea kombo Thomas Tuchel ndani ya PSG, athari yake inaweza kuwakumba Real Madrid katika mchakato wa kumsaka Kylian Mbappé.

Real Madrid walikuwa anajipanga kutumia mwanya wa Mbappé kutokuwa na mahusiano mazuri na Tuchel kama sehemu ya kuwavamia PSG majira ya kiangazi na kumsajili nyota huyo wa Ufaransa.

Thomas Tuchel

Baada ya kuwa na maneno ya mara kwa mara kati ya Thomas Tuchel na uongozi wa PSG, uongozi wa timu hiyo uliamua kumfuta kazi kocha huyo na sasa Madrid wajipange upya.

Inasemekana Mauricio Pochettino ananafasi kubwa ya kuwa kocha mpya wa PSG na ameahidiwa Kylian Mbappé sambamba na wachezaji nyota wengine wa kikosi hicho, hawatouzwa.

Kylian Mbappé

Kama taarifa hizi ni zakuaminika, ni dhahiri Florentino Perez na Zidane wameula wa chuya kwa kiasi kikubwa. Perez alikuwa akimtizama Pochettino kama mtu sahihi wa kukinoa kikosi cha Madrid endapo Zidane ataondoka au kitimuliwa klabuni hapo.

Zidane alikuwa anamtizama Mbappé kama miongoni mwa wachezaji wenye sifa ya kuwepo kwenye kikosi chake anachotarajia kukisuka upya.

Licha ya PSG kutaka kuendelea kumbakiza Mbappé, imeripotiwa kuwa kikosi cha mchezaji hiyo kinaamini kusaini mkataba mpya na timu hiyo inawezekana, endapo tu kama PSG wataweka kipengele cha kumuwezesha kujiunga na Madrid au timu nyingine yeyote itakapo hitaji kumsajili.

Mauricio Pochettino

Kwa taarifa za chini ya kapeti, PSG wanataka kuweka dau la pauni euro milioni 250 kwa timu yeyote itakayotaka kumsajili Mbappé. Real Madrid walijiandaa kuja na euro milioni 180 na hivyo hili huenda likawa ni pigo kwao.

Licha ya yote haya, swali ni – Je, Mbappé atachagua kubaki PSG baada ya Tuchel kufukuzwa au atataka kuondoka?


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

10 Komentara

    Inabidi psg wajipange upya

    Jibu

    Psg inabidi wabadilike sana

    Jibu

    Psg wajipange tu wabadilike

    Jibu

    Mbape madrid ni pahala pa mafanikio

    Jibu

    Mbappe fundi

    Jibu

    Changamoto kubwa sana kwenye kumpata Mbappe

    Jibu

    Mbappe mtumbaya

    Jibu

    Atakavyo yy ndo hvyo hvyo

    Jibu

    Real wangempata mbappe ingekuwa poa sana

    Jibu

    Mbappe fundi

    Jibu

Acha ujumbe