Klabu ya Real Madrid wamemaliza vinaya msimu huu baada ya kupokea kichapo cha 0-2 dhidi ya Real Betis kwenye gemu yao ya mwisho ndani ya Santiago Bernabeu.
Meneja Zinedine Zidane aliendelea na mbinu yake ya kubadili wachezaji kwa kuwabadilisha karibu nusu ya wachezaje waliosakata kabumbu kwenye gemu waliyopokea kichapo cha 3-1 dhidi ya Real Sociedad wiki iliyopita. Mbinu ya meneja huyu haikuzaa matunda.
Magoli yote yalichapwa kipindi cha pili kutoka kwa Loren Moron na Jese na kuwazawadia Real Betis ushindi wa bao 0-2.
Kazi kubwa ipo mbele ya Zidane kuwarudisha Real Madrid kwenye mstari, toka aliporejea klabuni hapo amejitahidi kufanya Santiago Bernabeu kuwa sehemu ambayo sio rahisi kuondoka salama akifanikiwa kukusanya pointi 15.
Gemu hii inachukuliwa kuwa inaweza kuwa ndiyo baibai kwa idadi kubwa ya wachezaji ambao wanatarajiwa kusepa msimu huu wa joto wakati meneja huyu akisuka upya kikosi kazi cha heshima kwenye dirisha la usajili. Bale na Navas ni moja kati wachezaji wanaotajwa kuwa huenda watasepa kwenye dirisha hili la usajili. Zidane amesikika akidai kuwa “tutafanya vyovyote ili kumuepuka Bale Msimu huu.
Povel tz
Duh majanga kwl