Real Madrid Wamepoteza €15m kwa Siku 4

Kwa mujibu wa  Marca, klabu ya Real Madrid imepoteza €15m ndani ya siku 4.

Real Madrid walikuwa na mfululizo wa mechi dhidi ya Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa, na nyingine dhidi ya Barcelona kule La Liga, lakini wametengeneza mapato kidogo ukifananisha na namna ambavyo huwa inakuwa katika hali ya kawaida.

Licha ya kupunguza matumizi, Real Madrid wameshindwa kutengeneza faida kutokana na kucheza mechi bila mashabiki.

Real Madrid Wamepoteza €15m kwa Siku 4
Mechi zenye mashabiki huwa na faida kubwa kwa vilabu na huwasaidia kujikimu kiuendeshaji.

Kucheza bila mashabiki ni suala ambalo limeanza kuzoeleka, mashabiki wakiendelea kutazama soka kwenye runinga zao bila kufika uwanjani kwa sababu ya janga la corona. Lakini, hali ni tofauti sana kwa vilabu, vikiwa vinapitia hali ngumu kiuchumi kwa sababu ya kukosa mapato.

Kwa mechi ya kawaida ambayo ingefanyika Santiago Bernabeu, El Classico pekee ingewatengenezea Madrid pesa kubwa. Rekodi zinataja kuwa mechi dhidi ya Liverpool ingeweza kuwaingizia takribani €10m, wakati El Classico yenyewe ingekuwa chini kidogo ya hiyo, lakini kiuhalisia hawajaweza kuingiza chochote na wanakadiriwa kupata hasara ya €15m.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

3 Komentara

    Madrid mbona mnatuangusha mashahiki

    Jibu

    Real Madrid wajipange upya

    Jibu

    Kutengeneza mapato kidogo ni kutokana na hali ya uchumi

    Jibu

Acha ujumbe