Real Madrid imekanusha uhusiano wowote na usajili wa Enzo Fernández, ikisema kuwa tetesi hizo “hazina msingi,” huku ripoti zikidai kuwa klabu moja ya EPL inajiandaa kutoa ofa ya rekodi kwa ajili ya Vinícius Júnior.

Katika mazungumzo yanayoendelea kuhusu mishahara ya wachezaji wanaolipwa zaidi. José Mourinho anamchukulia Federico Valverde kama mchezaji asiyeguswa.
Kuna pia ripoti zinazodai kuwa Madrid inaweza kupokea hadi euro milioni 12.5 kutokana na uhamisho wa Mario Gila, huku AC Milan ikikaribia kumsajili kwa takriban euro milioni 25. Real Madrid ina asilimia 50 ya haki za mchezaji huyo baada ya maendeleo yake akiwa SS Lazio.
Kuhusu Aurélien Tchouaméni, ripoti zinaeleza kuwa Real Madrid inaweza kuwa tayari kumuuza, huku vilabu vinavyotajwa kama Bayern, Chelsea, PSG, Manchester City na Manchester United vikitajwa kuonyesha nia. Manchester United inaonekana kuwa mbele zaidi iwapo uamuzi wa kumuuza utafanyika.



