Klabu ya Real Madrid mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa ulaya imeng’ara kwenye hafla ya droo ya ligi ya mabingwa ulaya iliochezeshwa jana saa moja usiku jijini Instanbul nchini Uturuki.

Hafla hiyo ya upangaji wa makundi ya timu zitakazoumana kwenye msimu wa 2022/23 wa michuano hiyo mikubwa barani ulaya.

real madrid, Real Madrid Yang’ara Usiku wa Droo za Ligi ya Mabingwa Ulaya., Meridianbet

Wakati shughuli ya upangaji wa makundi ikiendelea kulikua na shughuli ya ugawaji wa tuzo za wachezaji waliofanya vizuri kwa msimu wa 2021/22 ambapo Real Madrid ilitawala baada ya kutoa mchezaji bora wa ulaya ambae si mwingine Karim Benzema aliekua na msimu bora baada ya kuiwezesha timu yake kutwaa taji hilo la ulaya pamoja na kumaliza mfungaji bora wa michuano.

Pia Benzema ameshinda goli bora la msimu alilowafunga klabu ya Chelsea ya Uingereza kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Real Madrid iliendelea kung’ara kwenye usiku huo baada ya kocha wa klabu hiyo Carlo Anchelotti kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka wa ulaya mbele ya Pep Guardiola anayefundisha klabu ya Manchester City pamoja na Jurgen Klopp anayefundisha klabu ya Liverpool kocha Anchelotti amebeba tuzo hiyo baada ya kuisaidia klabu yake kubeba mataji kadhaa kama ligi ya mabingwa ulaya,La liga, Spanish supercup, pamoja na Uefa supercup.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa