Real Madrid Yashindwa Kupindua Meza Bernabeu

Jana michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya iliendelea ambapo mchezo ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu ni huu wa Real Madrid vs Arsenal ambao ulikuwa umeshika hisia za mashabiki mbalimbali.

Real Madrid Yashindwa Kupindua Meza Bernabeu

Real Madrid walikuwa na kibarua kizito cha kupindua meza kibabe nyumbani kwao mbele ya vijana wa Mikel Arteta ambao mchezo wa kwanza walishinda 3-0 pale Emirates, mabao yakifungwa na Declan Rice na Merino.

Licha ya Real kuanzisha mastaa wao kama Kylian Mbappe, Vinicius, Jude Bellingham, Rodrygo kwa upande wa ushambuliaji lakini bado hali ilikuwa ngumu kwao kwani walienda mapumzikao wakiwa hawana shuti lolote lililolenga lango.

Arsenal walipata penati kipindi cha kwanza, lakini Bukayo Saka alishindwa kuitanguliza The Gunners mbele baada ya Courtois kupangua mkwanju huo wa penati.

Dakika ya 65 Bukayo Saka aliitanguliza Arsenal mbele baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Merino, lakini dakika mbili mbele naye Vinicius aliisawazishia Madrid na kufanya ubao usomeke 1.-1, huku aggregate ikiwa ni 4-1.

Real Madrid Yashindwa Kupindua Meza Bernabeu

Kadi muda ulivyozidi kwenda ndipo mashabiki wa Real Madrid walivyozidi kukata tamaa kwani nafasi ya kupindua meza ilizidi kupungua, na dakika ya 93, mashabiki waliumia zaidi baada ya Martinelli kuingia kambani na hivyo kuwafanya mabingwa hao mara 15 wa michuano hii sio tuu kushindwa kufuzu, bali kushindwa kushinda pia mchezo.

Vijana wa Ancelotti wametolewa kwao kwa aggregate ya 5-1, na hivyo basi Arsenal wametinga Nusu Fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya ambapo watakutana na PSG. Je vijana hao wa London ambao hawajawahi kuchukua taji hili huu ndio wakati wao?

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.