Kocha wa zamani wa West Ham United, Harry Redknapp ametoa ushauri kwa timu hiyo kuwa wasijethubutu kumuacha mchezaji wao tegemezi Mark Noble pale ambapo mkataba wake utaisha.

Redknapp ambaye aliwahi kuwa kocha wa West Ham miaka ya 90’s mpaka mwanzon mwa 2000’s anadai kuwa amechunguza sana kikosi cha wagonga nyundo hao na anahisi kuwa mchezaji huyo ana umuhimu mkubwa sana kikosini hapo.

Noble aliongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kusalia klabuni hapo huku mkataba wake ukitegemewa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao.

Akizungumza na televisheni ya mashabiki wa West Ham United, Redknapp alisema kuwa kumuacha mchezaji kama Noble kutakuwa ni kupoteza kipaji muhimu na muhimili wa msingi katika kikosi cha the hammers.

Redknapp anaamini kuwa Noble ambaye amekuwa klabuni hapo toka mwaka 2003 anastahili kumaliza wakati wake pale West Ham kwani bado anavitu vingi sana vya kutoa kwenye timu.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa