Beki wa kulia na nahodha wa klabu ya Chelsea Reece James amerejea mazoezini baada ya kua nje ya uwanja kutokana na majeraha ambayo yalikua yanamsumbua beki huyo.

Reece James amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara hivo kurejea kwake mazoezini ndani ya klabu hiyo ni taarifa njema sana kwa timu na kocha wa klabu hiyo Mauricio Pochettino.reece jamesBeki huyo nahodha wa klabu hiyo amekua akiandamwa na majeraha sana ndani ya timu hiyo jambo ambalo limemfanya kukosa michezo mingi ya klabu hiyo, Vilevile mchezaji huyo amemaliza kifungo chake alichohukumiwa kwa kumtukana mwamuzi.

Beki huyo ni wazi ataweza kuwepo katika mchezo wa wikiendi ambapo klabu ya Chelsea itakipiga dhidi ya mahasimu wao kutoka jiji la London klabu ya Arsenal, Hivo kurejea kwa beki huyo ni wazi anakwenda kuongeza nguvu kuelekea mchezo huo.reece jamesAidha beki mwingine wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Ufaransa Axel Disasi ambaye alikua akisumbuliwa na majeraha madogo nae alionekana mazoezini, Hii ni dalili nzuri kwa klabu ya Chelsea kuelekea mchezo wao dhidi ya Arsenal ambapo Reece James na Axel Disasi watakuepo kwenye mchezo huo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa