Reece James Hatarajiwi Kurejea Karibuni

Nahodha wa klabu ya Chelsea Reece James iinaelezwa hatarajiwi kurejea kwenye kikosi hicho baada ya kua anasumbuliwa na majeraha ya misuli ambayo amepata wiki kadhaa zilizopita.

Reece James ilitarajiwa anaweza kurejea mwanzoni mwa mwezi Disemba lakini hali imekua tofauti kwakua mchezaji huyo hatarejea ndani ya muda huo kama ambavyo ilitarajiwa awali, Hivo beki huyo wa kimataifa wa Uingereza ataendelea kua nje ya uwanja kwa muda kidogo.Reece jamesMchezaji huyo amekua akipitia kipindi kigumu kwani kwa miaka miwili sasa amekua mchezaji wa kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara, Ikitokea amerejea uwanjani anachukua muda mchache kucheza na kurejea tena kwenye majeraha jambo ambalo hata yeye mwenyewe amekiri linamuumiza sana.

Beki Reece James amekua akiandamwa na majeraha mpaka sasa klabu ya Chelsea imezoea kucheza bila bila yeye kwakua walisajili beki wa kulia kutoka Olympique Lyon Malo Gusto ambae kwasasa ndio anavaa viatu vya Reece muda mwingi ambao amekua akikosekana kiwanjani.

Acha ujumbe