Reece James, Malo Gusto Bado Wana Majeraha

Wachezaji wawili wa Chelsea nahodha wa klabu hiyo Reece James pamoja na Malo Gusto bado wataendelea kua nje ya uwanja wakiendelea kuuguza majeraha yao ambayo waliyapata wiki kadhaa nyuma.

Beki Reece James amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara na kocha wa klabu hiyo Enzo Maresca amethibitisha kua wachezaji hao bado wataendelea kua nje ya uwanja kwa kipindi fulani ili kurejea kwenye utimamu wao na kuweza kuitumikia tena timu hiyo.reece james“Reece James bado hayupo na kupona kwake kumechelewa kidogo.”

“La muhimu zaidi ni kwamba warudi wakiwa na afya ya asilimia 100. Reece bado hayupo.” haya ni maneno ya kocha huyo wa ambaye ni mpya ndani ya klabu hiyo akitokea Leicester City.

Jambo la muhimu ambalo klabu hiyo wanaliangalia kwasasa ni kuhakikisha hawataharakisha kurejea kwa wachezaji waliopo majeraha haswa Reece James ili kuepusha kupata majeraha kwa mchezaji huyo, Kwani mara nyingi mchezaji akiwa hajapona vizuri na kurejeshwa uwanjani na ni rahisi kupata tena majeraha.

Acha ujumbe