Stephanie Frappart alikuwa muamuzi wa kike wa kwanza kuchezesha mechi kubwa ya wanaume Ulaya pale alipochezesha gemu ya fainali ya Uefa Super Cup kati ya Liverpool V Chelsea na agosti 14, 2019.

Mwanamama huyu alikuwa na wasaidizi wengine wanawake kwenye mechi hiyo. Stephanie pia alikuwa muamuzi kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake mwezi Julai 2019.

Raisi wa UEFA, Aleksander Ceferin alibainisha kuwa anafurahia uteuzi wake, kwa kuwa ni muendelezo wa usawa katika michezo. Anaamini atakuwa ni hamasa kwa wanawake wengi duniani hasa wasichana wenye ndoto kubwa kupitia mafanikio yake.

Stephanie Frappart aliungana na Manuela Nicolosi na Michelle O’Neill kwenye mechi hiyo.

Mwanamke, Refarii Mwanamke Kuchezesha Liverpool v Chelsea, Meridianbet
Stephanie Frappart, Manuela Nicolos na Michelle O’Nelll

Stephanie ambaye ni raia wa ufaransa mwenye umri wa miaka 35, pi alikuwa muamuzi wa kwanza mwanamke kusimamia mechi ya League 2 mwaka 2014, na kuwa muamuzi wa kwanza mwanamke kusimamia mechi ya Ligue 1 mwezi Aprili. Pia yupo kwenye orodha ya waamuzi watakaosimamia mechi za wanaume Ufaransa msimu wa 2019/20.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa