Rennes Wakanusha Ofa ya Camavinga Kutoka United

Mkurugenzi wa michezo wa Rennes, Florian Maurice amekataa madai kwamba Manchester United wamewasilisha zabuni kwa Eduardo Camavinga.

Kijana huyo wa miaka 18 anadaiwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaotafutwa sana sokoni huko Uropa msimu huu wa joto akiwa amebakiza miezi 12 tu kwenye mkataba wake.

United wameripotiwa kujiunga na Paris Saint-Germain na Real Madrid kusajili kuwania saini ya kijana huyo, ambaye anatarajiwa kuachana na gwanda la Ligue 1.

Camavinga: Ni Vizuri Kuhitajika na Vilabu Vikubwa.

Lakini, Maurice amekanusha kwa msisitizo uvumi kwamba Rennes tayari wamepokea ofa ya nyota ambaye ni miungoni mwa wachezaji wao wanayothaminiwa zaidi.

Akizungumza na TV Rennes, Maurice alisema: “Hakuna ofa iliyopokelewa kwa ajili ya Eduardo Camavinga, sio kutoka PSG wala kutoka Manchester United. Tunatulia juu ya hali yake. Najua hataki kuondoka bure.”

Wakati bei ya Camavinga imeripotiwa kuwekwa kwa pauni milioni 42, klabu tatu zinazomwinda zitajaribu kumshawishi Rennes kumuuza kwa bei ya chini.


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe