Atalanta imemsajili rasmi mshambuliaji wa kimataifa wa Italia Mateo Retegui kutoka Genoa kwa mkataba wenye thamani ya €28m ikijumuisha nyongeza.
Mshambuliaji huyo wa kati alipewa kipaumbele baada ya mchezaji mwenzake wa Azzurri, Gianluca Scamacca, kutengwa kwa miezi sita kwa kupata majeraha wakati wa mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu mpya.
Mzaliwa huyo wa Argentina, Retegui alifanyiwa vipimo asubuhi jana mjini Bergamo na kuweka bayana kwenye mkataba.
Alikuja Serie A kutoka Club Atletico Tigre hadi Genoa msimu uliopita wa joto kwa €15m pamoja na bonasi zinazohusiana na utendaji, ingawa baadhi ya hizo zitaenda kwa klabu yake ya zamani.
