Revocatus : Magoli Niliyofunga Nayafanyia Mazoezi.

 

Mfungaji wa mabao mawili ya Mwadui FC dhidi ya Yanga Aniceth Revocatus amesema, goli la shuti la mbali alilomtungua Shikhalo ni kitu ambacho huwa anakifanyia kazi awapo mazoezini.

Kabla ya kukutana na Yanga nilikuwa nawaza naenda kukutana na mabeki bora wawili wa kati nchini, nilikuwa nawaheshimu ndio maana nilifanikiwa kufunga.

 

β€œShuti nililopiga kufunga goli la pili ni kitu ninachokifanyia sana mazoezi, nimejaribu dhidi ya Yanga nikafanikiwa” alisema Revocatus.
Revocatus amesema hajaonekana kwenye mechi nyingi za VPL kwa sababu alipata majeraha mwanzoni mwa msimu hivyo alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
β€œWakati Ligi inaanza nilipata majeraha [enka] kwenye mechi za mwanzoni nikapona wakati raundi ya kwanza ya ligi inaelekea mwishoni. Nikarudi nikacheza dhidi ya KMC nikaumia tena lakini kwa sasa nipo sawa.” aliongeza

Revocatus amesajiliwa msimu huu kutoka GIPCO FC [kwa sasa Ken Gold FC] ikiwa Ligi Daraja la Kwanza.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe