Rio Ferdinand Apinga Bruno Kuvuliwa Unahodha

Beki mahiri wa zamani wa klabu ya Manchester United Rio Ferdinand amepingana na gwiji mwenzake wa zamani wa klabu hiyo Roy Keane juu ya kiungo Bruno Fernandes kuvuliwa unahodha klabuni hapo.

Rio Ferdinand amekuja na kupingana maoni aliyoyatoa Roy Keane baada ya kusema kua Bruno Fernandes hastahili kua nahodha wa klabu ya Manchester United kwasasa.rio ferdinandRoy Keane aliyazungumza hayo baada ya mchezo wa ligi kuu ya Uingereza ambapo Manchester United walipoteza dhidi ya mahasimu wao Manchester City, Huku Roy Keane akisema Bruno Fernandes anaenda kinyume na vigezo vyote vya kua nahodha.

Gwiji Rio Ferdinand amesema kocha Erik Ten Hag anakumbana na matatizo mengi ya nje ya uwanja akitolea mfano suala la Sancho, Mason Greenwood,Antony, bila kumsahau Maguire hivo haitakua na afya kama ataleta jambo lingine ambalo litaharibu utulivu wa timu.rio ferdinandNahodha Roy Keane anaamini Bruno Fernandes hastahili kua nahodha wa klabu hiyo kwasababu haonyeshi sifa za kua nahodha, Huku Rio akiona hakuna sababu ya kumvua kitambaa Bruno Fernandes kwani itaharibu hali ya hewa na utulivu klabuni hapo.

Acha ujumbe