Rio Ferdinand: Ununuzi wa United kwa Qatar Umekaribia

Gwiji na beki wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Rio Ferdinand amesema klabu ya Manchester United ipo kwenye hatua za mwisho kununuliwa na wamiliki wa Qatar.

Rio Ferdinand ameyazungumza hayo mchana wa leo akisema kutoka katoka vyanzo vyake vya kuaminika ununuzi wa klabu ya Manchester United upo karibuni na wanunuzi watakua kutoka Qatar ambao wamekua wakihusishwa kuinunua klabu hiyo wakiongozwa na Sheikh Jassim.Rio FerdinandBeki huyo wa zamani wa klabu hiyo anasema anaomba wamiliki wa klabu hiyo familia ya Glazers wahakikishe wanakamilishe mchakato huo haraka ili klabu hiyo iweze kufanya usajili vizuri katika dirisha hili kubwa ambalo limefunguliwa jana.

Klabu ya Manchester United iliwekwa sokoni kuanzia mwaka jana mwishoni na wamiliki wa klabu hiyo familia ya Glazers ambapo mchakato wa kuinunua klabu umedumu kwa takribani miezi sita, Huku taarifa zikieleza Glazers ndio wanakwamisha dili hilo kukamilika.Rio FerdinandRio Ferdinand pamoja na magwiji wengine wa klabu hiyo wamekua wakitamani Glazers waiachie timu hiyo kwani anaona ni kama wamefeli kuiongoza klabu hiyo siku za hivi karibuni na klabu hiyo imekua ikiporomoka siku hadi siku kiwanjani.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.