Mlinda mlango wa klabu ya Chelsea, Green ametangaza kutundika glovu zake baada ya kipindi cha mafanikio na kikosi cha klabu hiyo ya Chelsea. Amekuwa kikosini hapo kwa muda sasa akiwa kama mlinda mlango wa akiba lakini kwa sasa anaona kwamba umri wake umemtupa mkono kuendelea.
Japo ameweza kuwa kikosini hapo kwa muda ila hajaonekana mara kwa mara akiwa langoni, alikuwa ni sehemu ya walinda mlango wa klabu hiyo. Mbali na hilo ametangaza kipindi kizuri sana ambacho ni cha mafanikio makubwa kwa klabu hiyo ambayo angalau wana taji mkononi.
Nyota huyo mwenye miaka 39 alikuwa na safari nzuri ndani ya klabu ya Leeds kwenye msimu wa 2016/17 wakiwa katika kampeni ya kutafuta nafasi ya kuipandisha klabu hiyo ili iweze kusogea juu ya ligi na kuweza kuwa sehemu ya mafanikio lakini mambo hayakwenda sawa kwao.
Mwaka 2017 alijiunga na Huddersfield akiwa kama mchezaji wa aina yake kwa kupata nafasi ya kuisogeza klabu yake hiyo katika hatua fulani nzuri ndani ya ligi hiyo pamoja na kwamba hakuwa chaguo la kwanza ndani ya kikosi hicho lakini aliweza kuvumilia kukaa kikosini hapo kwa wakati wote.
Japo hata ndani ya Chelsea hajapata nafasi ya kuonesha uwezo wake labda kutokana na ushindani mkubwa uliopo kati ya walinda mlango lakini ametangaza nafasi hiyo ya kuachana na kikosi hicho kwa kustaafu soka akiwa hana michezo aliyopewa kuisukuma klabu hiyo kwenye historia yake.
Ndani ya barua yake ameshukuru kila mmoja aliyekutana naye na kusaidiana naye wakati wote na kwa kipindi chote kwa sababu amecheza na kushinda na kwake anaamini yeye ni nyota wa soka duniani na mwenye heshima kubwa sana kwenye soka.
Safari yake aliianza ndani ya Norwich City ambako alikuwa sehemu ya mafanikio makubwa ndani ya kikosi hicho na baadaye akaingia West Ham kwa mafanikio kabla ya kutimkia QPR ambako pia alkuwa msaada mkubwa kabla hajaenda kujiunga na Leeds na baadaye Huddersfield na Chelsea hadi anastaafu.
Povel
Gud news