Legendari wa Real Madrid Roberto Carlos amesema kuwa Marcelo amekuwa mchezaji bora zaidi Madrid zaidi yake.

Marcelo anaonekana kumalizana muda wake na Real Madrid, huku wapenzi wa michezo wakiendelea kutathmini kushuka kwa kiwango chake na nafasi yake Real Madrid huku wengi wakiamini amekuwa mmoja wa wachezaji bora wa wakati wote.

Wakati staa huyu akiongoza kwa kuwa na medali nyingi zaidi kuliko mchezaji yeyote wa Real Madrid, Roberto Carlos alipata nafasi ya kumzungumzia nyota huyu.

“Soka lake limekuwa bora zaidi kuliko mimi. Wazi kuwa amekuwa bora. Ni mfano akiwa nje na ndani ya uwanja. Ni kiongozi. Ninafurahi kupata nafasi ya kumuona Marcelo akikua. Alichokifanya hapa, na akiwa na Brazil ni kukibwa”

Roberto Carlos

Carlos, alizungumza hayo kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa, ambayo Real Madrid wanavaana na Liverpool. Mkataba wa Marcelo unaisha mwisho wa msimu huu, na amekuwa akisikika juu ya nia yake ya kusalia Real Madrid lakini mpaka sasa hakuna ofa ambayo imewekwa wazi juu yake.

Marcelo

Roberto Carlos, ambaye amewahi kucheza na staa huyu anasema kuwa kila mmoja anampenda Marcelo klabuni Real, na yeye atazungumza na rais wa klabu ili kujua nini kitafanyika kwa kuzingatia mchango wa staa huyu.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa