Robertson Kufanyiwa Upasuaji

Beki wa kushoto wa klabu ya Liverpool raia wa kimataifa wa Scotland Andy Roberson anatarajia kufanyiwa upasuaji baada ya kupata jeraha la bega amethibitisha kocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp.

Kocha Jurgen Klopp amesema beki Robertson atakua nje ya uwanja kwa muda kidogo kutokana na majeraha ambayo ameyapata na kumfanya kufanyiwa upasuaji.RobertsonBeki huyo alipata majeraha hayo wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Scotland katika mchezo wa kufuzu michuano ya mataifa ya ulaya yanayotarajiwa kufanyika nchini Ujerumani mwaka 2024.

Beki huyo ni wazi atakosa mchezo wa derby ya Merseyside kesho kati ya klabu ya Liverpool na Everton katika mchezo unaotarajiwa kupigwa katika dimba la Anfield mapema kabisa kesho.RobertsonBeki Robertson ni wazi ataacha pengo kubwa ndani ya klabu ya Liverpool katika kipindi ambacho atakua nje ya uwanja, Kwani beki huyo amekua msaada kwa klabu hiyo kwa kipindi kirefu ndani viunga vya Anfield kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha.

Acha ujumbe