James Rodriguez ambaye ni raia wa Colombia na mwenye umri wa miaka 31 amejiunga na timu ya Ugiriki inayojulikana kama Olympiacos akitoka katika klabu ya Al Rayyan. Mchezaji huyo anacheza kama kiungo mshambuliaji.

 

Rodriguez Ajiunga na Olympiacos

Mchezaji huyo amewahi kucheza vilabu mbalimbali ikiwemo Monaco katika mwaka wa 2013-2014 , akacheza Bayern Madrid na Everton ya Uingereza kabla ya kwenda Al Rayyan ya huko Qatar.

Dili hilo sasa limekamilika baada ya vipimo vilivyofanywa siku ya Jumatano, James atatambulishwa kama mchezaji wa Olympiacos leo baadae. Baada ya Marcelo na James Rodriguez mchezaji atakayesajiliwa kwenye klabu hiyo atakuwa ni Cedric Bakambu  ambaye atajiunga kwa mkataba wa kudumu kutoka Olympique Marseille.

 

Rodriguez Ajiunga na Olympiacos

Olympiacos katika ligi ya Ugiriki wamecheza michezo minne, wameshinda miwili, wametoa sare na hawajapoteza mchezo wowote. Wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo huku wakiwa na alama 8 wakipitwa alama mbili na kinara wa ligi ambaye ni Panathinaikos.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa