Roma wamethibitisha rasmi kumsajili mshambuliaji kijana mwenye kipaji kikubwa Robinio Vaz kwa uhamisho wa kudumu kutoka Marseille.

Taarifa ya klabu ya Ufaransa imethibitisha maelezo ya kifedha ya dili hilo, yenye thamani ya €25 milioni ikijumuisha bonasi, pamoja na asilimia 10 ya ada ya mauzo ya baadaye.
Katika taarifa iliyotolewa na klabu, Roma walitangaza kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18 amesaini mkataba wa miaka minne utakaomalizika Juni 2030. Vaz anawasili katika mji mkuu baada ya kujitokeza kama mmoja wa vipaji vinavyoongoza katika safu ya ushambuliaji kwa rika lake nchini Ufaransa.
Alifanya debut yake ya timu ya wakubwa chini ya kocha Roberto De Zerbi Januari mwaka jana, akicheza katika mechi ya Coupe de France dhidi ya Lille.
Vaz baadaye alicheza kwa mara ya kwanza Ligue 1 msimu huo na pia amepata uzoefu katika kampeni ya UEFA Champions League msimu huu.


