Roma Wamgeukia Antonio Nusa

AS Roma wako kwenye harakati za kusaka winger mpya, na macho yao sasa yameelekezwa kwa Antonio Nusa wa RB Leipzig. Kwa mujibu wa Gazzetta dello Sport, Waroma wamewasiliana na uongozi wa Leipzig kuhusu uwezekano wa usajili.

Roma Wamgeukia Antonio Nusa

Nusa, mwenye umri wa miaka 21, alijiunga na Leipzig kutoka Club Brugge majira ya kiangazi ya 2024 kwa ada ya €21m na haraka akawa mchezaji wa kikosi cha kwanza. Msimu uliopita alicheza mechi 35 na kufunga mabao 5 pamoja na kutoa asisti 4. Hata hivyo, Leipzig hawako tayari kumwachia kirahisi, wanataka kati ya €50m–€60m, huku mkataba wake ukidumu hadi 2029.

Roma wanamwona Nusa kama suluhisho baada ya Mason Greenwood kujiunga na Fenerbahce na Crysencio Summerville kuhamia Al-Hilal. Lakini pia wanaangalia majina mengine, Andreas Schjelderup wa Benfica pamoja na Said El Mala, chipukizi wa Cologne mwenye miaka 19, anayevutwa pia na Borussia Dortmund.

Roma Wamgeukia Antonio Nusa

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Nusa pia anavutia klabu nyingine kama Newcastle United, Arsenal, Juventus, Tottenham Hotspur na Crystal Palace. Bayern Munich walihusishwa awali, lakini walishamaliza usajili wa Ismael Saibari kutoka PSV.

Roma Wamgeukia Antonio Nusa

Kwa sasa, sakata hili linaendelea kuwa vita ya usajili barani Ulaya. Roma wanahitaji winger mpya haraka, lakini bei kubwa ya Leipzig na ushindani mkali kutoka klabu zingine vinawafanya wapime chaguo lao kwa makini.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.