Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ametangaza kuiacha klabu hiyo mikononi mwa bodi ya wadhamini kutokana na sakata linaloendelea vita kati ya Ukraine na Urusi.

 

Abramovich, Roman Abramovich Aikabidhi Chelsea kwa Bodi ya Wadhamini., Meridianbet

Hali hiyo imepelekea mataifa mengi makubwa kufungia wafanyabiashara wakubwa kutoka Urusi kufanya nao biashara pamoja na vikwazo mbalimbali.

Hii imepelekea Mmiliki wa Chelsea ambaye inasemekana ni moja kati ya watu wa karibu wa Rais Putin, Roman Abramovich kuamua kujitenga na klabu kwa muda na kuwapa nafasi bodi ya wadhamini kuendelea na shughuli za klabu hiyo.

Katika taarifa yake, bilionea huyo wa Urusi alisema: “Wakati wa umiliki wangu wa karibu miaka 20 wa Chelsea FC, siku zote nimekuwa nikitazama jukumu langu kama mlezi wa klabu, ambayo kazi yake ni kuhakikisha kwamba tunafanikiwa kadri tuwezavyo leo, pamoja na kujenga kwa ajili ya siku zijazo, huku pia tukiwa na nafasi chanya katika jamii zetu.

“Siku zote nimekuwa nikichukua maamuzi kwa nia ya dhati ya klabu. Ninasalia kujitolea kwa maadili haya. Ndiyo maana leo ninawapa wadhamini wa msingi wa hisani wa Chelsea uwakili na utunzaji wa klabu ya Chelsea FC.

“Ninaamini kwamba kwa sasa wako katika nafasi nzuri ya kuangalia maslahi ya klabu, wachezaji, wafanyakazi na mashabiki.” aliongeza Abramovich.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa