Mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan Romelu Lukaku yuko shakani kukosa mechi ya watani wa jadi wikiendi ijayo kwenye dabi ya Della Madonnina kutokana na majeruhi.

Romelu Lukaku ameondolewa kwenye kikosi cha Inter Milan ambacho kitacheza na Cremonese katika ya wiki hii kutokana na kupata majera ya nyonga.

Romelu Lukaku, Romelu Lukaku Kuwakosa  AC Milan, Meridianbet

Romelu Lukaku alipata majeraha hayo kwenye mazoezi ya asubui jumapili baada ya kikosi hicho kutoka kwenye kipigo cha 3-0 dhidi ya Lazio siku ya Ijumaa jioni, pia lukaku anatarajia kukosa mchezo wa ligi ya mabingwa wa ufunguzi dhidi ya Bayern Munich kati kati ya wiki ijayo.

Hizi ni habari mbaya kwa kocha Simone Inzaghi ambaye anataka kuuwasha tena moto wa safu hiyo ya ushambulliaji kwa kuwaunganisha tena Lukaku na Lautaro Martinez.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa