Klabu ya Manchester United imemuacha mshambuliaji wake nyota Cristiano Ronaldo kwenye kikosi kilichoondoka leo kwenda Norway kwa ajiri ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Atlético Madrid.

Ronaldo ajacheza mchezo wowote wa Pre-season mpaka sasa na imetarifiwa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno anatafuta timu ambayo inashiriki ligi ya mabingwa ulaya ili awe kucheza michuano hiyo msimu huu.

Ronaldo, Ronaldo Aachwa Kwenye Mechi Dhidi ya Atlético Madrid, Meridianbet

Manchester United inatarajia kucheza na Atlético Madrid jijini Oslo siku ya Jumamosi kwenye wa mchezo wa kirafiki, na siku ya jumapili watacheza mchezo wa fainali dhidi ya Rayo Vallecano, kabla ya ufunguzi wa michezo ya Premier League dhidi ya Brighton Agosti 7.

“Baadhi ya wachezaji kwenye kikosi cha chetu watakosekana, ambao utachezwa siku ya jumamosi na mchezo wa jumapili dhidi ya Rayo Vallecano, wakati wachezaji wengine wakiwa wagonjwa au majeruhi.” Man Utd walisema wakihusianisha na mchezo dhidi ya Atlético Madrid.

Manchester United mpaka sasa hawajathibitisha ikiwa Ronaldo atakuwepo kwenye kikosi cha kitakacho cheza dhidi ya Rayo Vallecano.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa