Bila shaka miongoni mwa majina ya wachezaji wakubwa sana duniani, Cristiano Ronaldo ni jina ambalo haliwezi kosekana. Jamaa anajua kukiwasha licha ya sehemu anayofikiaga.

Kocha wa zamani wa timu za Madrid, Chelsea, United, Tottenham na sasa As Roma, Jose Mourinho ameelezea maono yake juu ya Cristiano Ronaldo, huku akimtaka aondoke Serie A tu amuache awe na amani.

Mourinho anamuelezea CR7 kama mtu ambaye anajituma sana licha ya umri wake kuwa umeenda sana lakini bado anatamani kuendelea kuvunja rekodi kila siku na kujitengenezea jina lake katika historia ya soka.

Ronaldo aweka rekodi
Ronaldo akishangilia goli na Mourinho
Hivi karibuni tu akiwa na Juventus kwa misimu mitatu, Ronaldo amefikisha jumla ya mabao 100 katika ligi hiyo akiwa na Serie A na msimu huu tu ameshinda tuzo ya mfungaji bora akiingia kambani mara 29.
ronaldo
Ronaldo akishangilia goli lake la 100 Juventus

Mourinho anamuona Cristiano kama mtu anayetamani changamoto kila siku na kupata wakosoaji ili aendelee kuwaonesha uwezo wao mkubwa wa kusakata kabumbu na kuendelea kuvunja rekodi.

Mourinho hivi sasa ni kocha wa Roma na ataenda kukutana na Cristiano katika upande mwingine katika mbio moja ya kusaka taji la Serie A, hivyo Mourinho anatamani mchezaji huyo akapumzike kwingine huko.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa