Ronaldo Anawatisha Wenzake United?

Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wanaripotiwa ‘kuogopa mawazo’ ya Cristiano Ronaldo pale Old Trafford.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 alinukuliwa katika mahojiano na Sky Sports News kwamba kila mchezaji wa Red Devils anaweza kufanya vizuri zaidi na hatakubali klabu hiyo kumaliza chini ya nafasi ya tatu kwenye Premier League.

Kuna ripoti ya hapo awali ilidai kuwa ujio wa fowadi huyo umesababisha mvutano kwenye chumba cha kubadilishia, ikidau uwepo wa makundi kadhaa vidogo kutokana na hilo.

Ronaldo
Cristiano Ronaldo

Kwa mujibu wa The Sun, wachezaji kadhaa wa United wanahofia kufanya makosa au kushindwa kutoa pasi sahihi kwa Ronaldo kwa sababu ya hisia mbaya wanayoweza kupata kutoka kwa mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or.

Ripoti hiyo pia inadai kuwa Ronaldo amenukuliwa akiwaambia wachezaji wachanga wa United: “Ikiwa hutaki msaada wangu, fanya kazi yako.”

Wachezaji wa kikosi cha kwanza cha United wanadaiwa kuwa wanapata wakati mgumu kufurahia mazoezi bila ushindani mkali ikilinganishwa na Ronaldo, ambaye anataka kutumia mbinu kadhaa zilizotumiwa hapo awali na gwiji wa klabu Sir Alex Ferguson.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe