Mchezaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amerejea mazoezini na timu ya kwanza baada ya kupewa adhabu siku kadhaa zilizopita baada ya kuonesha utovu wa nidhamu katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.ronaldoMchezaji huyo siku kadhaa kupitia taarifa ya klabu hiyo ilimsimamisha mchezaji huyo kwa kitendo chake cha kutoka uwanjani kabla ya mchezo kumalizika katika dimba la Old Trafford ulioshuhudia Man United ikiifunga klabu ya Tottenham mabao mawili kwa bila na staa huyo kutoka uwanjani kabla ya mchezo kumalizika kwa sababu zilizoelezwa ni kutokana na kukosa nafasi ya kucheza katika mchezo huo.

Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ameonekana mazoezini kwa mara ya kwanza akifanya mazoezi na timu ya wakubwa baada ya kukosa mchezo uliopigwa wikiendi dhidi ya Chelsea Man United wanajiandaa kucheza mchezo wao wa Uefa Europa League dhidi ya Sheriff.ronaldo, Ronaldo Arejea Mazoezini baada ya Adhabu., MeridianbetRonaldo amekua kwenye wakti mgumu msimu kwenye kikosi cha United baada ya ujio wa kocha mpya Eric Ten Haag ambae amekua hampi nafasi ya kutosha mchezaji huyo na pia ameonekana sio mchezaji ambae anafiiti kwenye falsafa za mwalimu wa zamani wa klabu ya Ajax.

Ukiachana na kurejea kwa Ronaldo mazoezini pia jambo ambalo limewavutia mashabiki wa timu hiyo ni kurejea kwa mshambuliaji wao raia wa Ufaransa Anthony Martial baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Everton wiki mbili kadhaa zilizopita.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa