Wadau wengi wa soka wanajiuliza kituo kinachofuata kwa Cristiano Ronaldo ni kipi msimu ujao? Ikumbukwe amebakiza mwaka 1 kwenye mkataba wake na Juventus mpaka sasa.

CR7 alijiunga na Juventus akitizamwa kama mkombozi atakayewapatia Juve kombe la Uefa. Mambo yamekuwa tofauti sana, kwa msimu huu pekee, Juve wanahatihati ya kuyakosa mashindano ya Uefa msimu ujao, tayari wamevuliwa ubingwa wa Serie A walioutawala kwa miaka 9 mfululizo.

Juventus haohao wapo kwenye hatari ya kupigwa rungu zito na Serie A endapo wataendelea kubaki kwenye mpango wa European Super League mpaka msimu ujao. Huenda wakaondolewa kabisa kwenye timu zinazoshiriki Serie A msimu ujao kama hawatojitoa kwenye mpango huo.

Ronaldo, Ronaldo Atarejea Nyumbani, Sporting CP?, Meridianbet
Licha ya kuwa na msimu mbaya kama klabu (Juventus), CR7 amefikisha jumla ya magoli 100 akiwa na klabu hiyo.

Ni vurugu tupu ndani ya Juventus kuelekea msimu ujao. Licha ya kuendelea kushikilia nafasi yake kama mchezaji bora duniani akichuana vikali na Lionel Messi, pengine huu ni muda wa Ronaldo kurudi nyumbani?

Akiwa na umri wa miaka 36, Ronaldo anahusishwa na uwezekano wa kuondoka Juventus mwishoni mwa msimu huu. Nyumbani kwako, Ureno kumeanza fununu kuwa mchezaji huyo anaweza akarudi kwenye Primeira Liga. Ligi iliyompatia nafasi ya kuonesha uwezo wake na akasajiliwa na Man United, safari yake ya ubora duniani ilianzia Sporting Lisbon.

Ronaldo, Ronaldo Atarejea Nyumbani, Sporting CP?, Meridianbet
Safari ya CR7 katika ubora wa dunia ilianzia Sporting CP

Japo ni watu wachache sana wanaoweza kumshauri CR7 katika maamuzi yake, mama yake mzazi amenukuliwa akisema atajaribu kumshauri mwanae kurudi Sporting CP msimu ujao.

Dolores Aveiro ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo, akiwa kwenye eneo la nyumbani kwake, aliwaambia mashabiki wa Sporting CP ambao walikuwa wakishangilia ubingwa wao msimu kuwa “nitajaribu kuongea nae (Cristiano Ronaldo) ili kumrudisha. Msimu ujao atakuwa akicheza Alvalade (uwanja wa Sporting CP)”


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Ronaldo, Ronaldo Atarejea Nyumbani, Sporting CP?, Meridianbet

CHEZA HAPA

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa