Mshambuliaji wa klabu ya Al Nassr na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuhakikisha klabu yake inapata alama tatu muhimu baada ya kufunga bao la ushindi katika mchezo wao dhidi ya Al Tai.
Ronaldo amefunga bao la ushindi dakika za jioni kabisa akihakikisha Al Nassr inaibuka kidedea na kuchukua alama tatu katika ligi kuu nchini Saudia Arabia jioni ya leo.Klabu ya Al Nassr ilianza vibaya ligi kuu ya Saudia Arabia maarufu kama Saudian Pro League msimu huu, Lakini imefanikiwa kurudi kwenye mstari katika michezo yake ya hivi karibuni kwa kupata matokeo ya ushindi.
Al Nassr walionekana kuitaka mechi kuanzia dakika ya kwanza kwani walikua wakifanya mashambulizi ya hapa na pale na kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa,Jambo ambalo lilichangia kuwapa bao dakika ya 32 ya mchezo likifungwa na Talisca.Kipindi cha pili Al Taio walirudi kwa kasi wakihitaji kusawazisha bao ambapo walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 79 ya mchezo kabla ya mwamba Cristiano Ronaldo kufunga bao la ushindi dakika ya 87, Huku Al Nassr wakipanda mpaka nafasi ya 3 ya msimamo wa ligi na alama zao 18.