Ronaldo Hajamalizana na Ten Hag

Gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo inaonekana bado ana dukuduku na kocha wa klabu ya Manchester United kwani ameendelea kumtupia madongo kocha Erik Ten Hag kupitia chaneli yake ya You Tube.

Ronaldo amemkosoa kocha Ten Hag kutokana na kauli yake aliyosema klabu hiyo haijakua tayari kubeba taji la ligi ya mabingwa ulaya pamoja na ligi kuu ya Uingereza, Jambo ambalo staa huyo amelipinga kwa kusemaronaldo“Meneja wa Man United… huwezi kusema kwamba hautapigania kushinda Ligi Kuu au Ligi ya Mabingwa.”

“Lazima useme hivi: labda hatuna uwezo wa kutosha, lakini tutajaribu. Lazima ujaribu!

Staa huyo wa zamani wa klabu hiyo ikumbukwe aliondolewa ndani ya klabu ya Man United na kocha Erik Ten Hag akitajwa kama mtu aliyehusika kwa kiwango kikubwa kumuondoa staa huyo ndani ya klabu hiyo, Kwani hilo lilithibitika alipohojiwa na kituo kimoja nchini Uingereza na kusema alipata usingizi mzuri siku alipofanikiwa kumundoa staa huyo ndani ya timu hiyo.

Ronaldo hakuishia hapo kwani alisema kocha huyo kama anataka kufanikiwa ndani ya timu hiyo amtumie staa wa zamani wa klabu hiyo ambaye yupo kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo

“Iwapo Ten Hag atamsikiliza Ruud van Nistelrooy… labda anaweza kumsaidia.”

“Anaujua klabu na klabu inapaswa kuwasikiliza wale waliokuwepo.”

“Rio, Roy Keane, Scholes, Gary Neville, Sir Alex Ferguson.”

“Huwezi, huwezi kujenga upya klabu bila maarifa.”

Acha ujumbe