Ronaldo Kuachana na Ureno Baada ya Miaka 20

Baada ya miaka 20 ya kuitumikia timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ni wazi sasa nyota huyo ataachana na timu ya taifa ya Ureno baada ya jana kutupwa nje kwenye michuano ya Euro 2024.

Stori ya Ronaldo na Ureno imekua na simulizi tamu na chungu kwa wakati mmoja tangu acheze mchezo wake wa kwanza akiwa na jezi ya taifa hilo mnamo Agosti 20 mwaka 2003 dhidi ya Khazakhstan, Tangu hapo nyota huyo amekua mkombozi mkubwa sana wa taifa hilo kwa miaka yote aliyoitumikia.ronaldoGwiji huyo amefanikiwa kuweka heshima kubwa sana kwenye taifa la Ureno ambapo amefanikiwa kuipatia mataji mawili makubwa kwa kipindi chote ambacho ameitumikia timu hiyo, Huku timu hiyo ikiwa haijawahi kutwaa taji kubwa lolote kabla ya gwiji huyo kuanza kuitumikia timu hiyo.

Siku kadhaa Staa huyo wa zamani wa Real Madrid alieleza michuano hii ya Euro 2024 itakua ya mwisho kwake na kimahesabu ni wazi mchezaji huyo hatakuepo mwaka 2026 kwenye michuano ya kombe la dunia itakayopigwa nchini Marekani na Canada hivi inawezekana jana akawa amecheza mchezo wake wa mwisho na timu ya taifa ya Ureno.ronaldoStaa Cristiano Ronaldo anaondoka timu ya taifa ya Ureno akiwa ameshinda taji la Euro mwaka 2016 na taji la Uefa Nations League 2019, Lakini pia anaondoka kwenye taifa hilo kama mfungaji bora wa muda wote mchezaji huyo anahesabiwa kama mchezaji bora wa muda wa taifa hilo kutokana na mafanikio ambayo ameipatia taifa la Ureno.

Acha ujumbe