Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo leo amerejea kwenye uwanja wa Carrigton leo baada ya kushindwa kuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kichocheza dhidi ya Leicester city siku ya Jumamosi.
Ronaldo alishindwa kufanya mazoezi ya na timu siku ya ijumaa jioni na kutokana na ugonjwa, Ralf Rangnick ilibidi abadilishe mfumo kwa kumuondoa kikosini baada ya klabu hiyo kutuma daktari wa timu nyumbani kwake siku ya jumamosi kuangalia uwezekano wa kuwepo kwenye kikosi.
Leo kocha wa klabu ya Manchester United Ralf Rangnick hiyo amethibitisha Ronaldo kurudi kwenye kikosi cha kwanza leo, na amefanya mazoezi ya pamoja na timu na anatarajia kumjumuisha kwenye kikosi kitakacho menyana na Everton kwenye mchezo wa wikiendi hii.
Pia leo baada ya kurudi kwenye kikosi na amaefanikiwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa klabu kwa mwezi march, baada ya kufunga magoli matatu murua dhidi ya Tottenham.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.