Supastaa wa klabu ya Al Nassr na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo anaendelea kuwasha moto kadri siku zinavyoendelea kwenda licha ya umri wake kuonekana kumtupa mkono.
Cristiano Ronaldo jana aliingia kwenye kitabu cha wafungaji wa mabao katika mchezo kati ya Ureno na Leichtenstien ambapo aliisaidia timu yake kushinda mchezo huo.Mchezo huo wa kufuzu michuano ya Euro 2024 ambapo Ureno walishinda kwa mabao mawili kwa bila, Huku supastaa huyo akifunga moja ya mabao katika mchezo huo na lingine kufungwa na Joao Cancelo.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Real Madrid, Man United, na Juventus licha ya umri wake wa miaka 38, Lakini amekua akiendelea kuushangaza ulimwengu kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha.Cristiano Ronaldo baada ya mchezo wa jana amefanikiwa kufunga mabao 10 katika michezo nane ya mwisho aliyoitumikia timu ya taifa ya Ureno, Huku akifanikiwa kufikisha mabao 108 katika michezo ya ushindani ya timu ya taifa hii ikiendelea kuonesha namna staa huyo ana njaa ya mafanikio na hataki kupoa.