Mshambuliaji wa Klabu ya Manchester United, Cristiano Ronaldo amewalazimisha wafanyakazi wa United kuboresha bwawa la kuogelea la timu hiyo baada ya kulalamika kwamba ’tiles zimelegea na kukatika katika kiasi kwamba ni hatari kwa usalama kwenye viunga hivyo vya mazoezi Carrington.
Ronaldo
Ronaldo

Ronaldo amegundua kuwa bwawa hilo la kuogelea halijabadilika tangu mwaka 2009. Nyota huyo amerejea Manchester United msimu uliyopita baada ya kutokuwepo hapo Old Trafford kwa miaka 12, alipojiunga na Real Madrid.

Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror, Ronaldo aliwaambia mabosi kwenye uwanja wao wa mazoezi wa ‘Aon’ kwamba hayuko tayari kutumia bwawa lao kuu au bwawa la kuogelea hadi yote mawili yarekebishwe, kwani alidai kuwa ’tiles zimelegea, chakavu na kukatika katika hivyo ni hatari kwa usalam.

Maofisa wa United walichukua malalamiko yake kwa uzito mkubwa na mara moja wakaamuru kazi za kurekebisha katika mabwawa hayo mawili zianze mara moja, ambayo yatakamilika kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya katikati ya Julai.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa