Cristiano Ronaldo amerejea mazoezini na Manchester United Jumatano baada ya kupewa likizo ya msiba kabla ya mechi ya Jumanne ya Ligi Kuu dhidi ya Liverpool.
Ronaldo hakuwepo kwenye kikosi kilichopokea kipigo cha 4-0 cha Man United dhidi ya Liverpool siku ya Jumanne.
Fowadi huyo alipigwa picha kwenye uwanja wa mazoezi wa timu yake Jumatano asubuhi, na kulingana kwa mujibu wa Manchester Evening News, alikamilisha kikao kamili.
Kutokana na hali hiyo, kuna uwezekano kuwa chipukizi huyo wa zamani wa Sporting Lisbon akawepo kwenye kikosi cha Man United kwenye Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Arsenal Jumamosi.

Mashabiki wa Liverpool na Man United walijumuika pamoja kwa kupiga makofi kwa dakika moja katika dakika ya saba ya pambano hilo lililofanyika Jumanne kwenye Uwanja wa Anfield kama ishara ya kumuunga mkono Ronaldo na familia yake.
Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!